1 Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami,
2 Chukua ngao na kigao.
3 Inua mkuki wako na fumo lako
4 Wafedheheshwe na waaibishwe
5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
6 Njia yao na iwe giza na ya utelezi,
7 Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu,
8 maafa na yawapate ghafula:
9 Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana
10 Nitapaza sauti yangu nikisema,
11 Mashahidi wakatili wanainuka,
12 Wananilipa baya kwa jema
13 Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia
14 niliendelea kuomboleza
15 Lakini nilipojikwaa,
16 Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki,
17 Ee Bwana, utatazama mpaka lini?
18 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,
19 Usiwaache wale wanaonisimanga,
20 Hawazungumzi kwa amani,
21 Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha!
22 Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya.
23 Amka, inuka unitetee!
24 Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu,
25 Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!”
26 Wote wanaofurahia dhiki yangu
27 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki
28 Ulimi wangu utanena haki yako