1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
2 Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi,
3 na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji.
4 Huzifanya pepo kuwa wajumbe wake,
5 Ameiweka dunia kwenye misingi yake,
6 Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi,
7 Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia,
8 yakapanda milima, yakateremka mabondeni,
9 Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka,
10 Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni,
11 Huwapa maji wanyama wote wa kondeni,
12 Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji,
13 Huinyeshea milima kutoka orofa zake,
14 Huyafanya majani ya mifugo yaote,
15 divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu,
16 Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri,
17 Humo ndege hufanya viota vyao,
18 Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu,
19 Mwezi hugawanya majira,
20 Unaleta giza, kunakuwa usiku,
21 Simba hunguruma kwa mawindo yao,
22 Jua huchomoza, nao huondoka,
23 Kisha mwanadamu huenda kazini mwake,
24 Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi!
25 Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele,
26 Huko meli huenda na kurudi,
27 Hawa wote wanakutazamia wewe,
28 Wakati unapowapa,
29 Unapoficha uso wako,
30 Unapopeleka Roho wako,
31 Utukufu wa Bwana na udumu milele,
32 yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka,
33 Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote;
34 Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,
35 Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia