Jeremias 3

SWHONEN

1 “Kama mtu akimpa talaka mkewe,

2 “Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone.

3 Kwa hiyo mvua imezuiliwa,

4 Je, wewe hujaniita hivi punde tu:

5 je, utakasirika siku zote?

6 Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Bwana aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko.

7 Mimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya yote haya angelinirudia, lakini hakurudi, naye dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili.

8 Nilimpa Israeli asiye mwaminifu hati yake ya talaka, na kumfukuza kwa ajili ya uzinzi wake wote. Hata hivyo nikaona kuwa Yuda dada yake mdanganyifu hakuogopa. Yeye pia alitoka na kufanya uzinzi.

9 Kwa sababu uasherati wa Israeli haukuwa kitu kwake, Yuda aliinajisi nchi kwa kuzini na mawe na miti.

10 Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema Bwana.

11 Bwana akaniambia, “Israeli asiye mwaminifu ana haki kuliko Yuda mdanganyifu.

12 Nenda, ukatangaze ujumbe huu kuelekea kaskazini:

13 Ungama dhambi zako tu:

14 “Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema Bwana. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni.

15 Kisha nitawapeni wachungaji wanipendezao moyo wangu, ambao watawaongoza kwa maarifa na ufahamu.

16 Katika siku hizo, idadi yenu itakapokuwa imeongezeka sana katika nchi, watu hawatasema tena, ‘Sanduku la Agano la Bwana,’ ” asema Bwana. “Halitaingia tena kwenye mawazo yao wala kukumbukwa, hawatalihitaji wala halitatengenezwa jingine.

17 Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha Bwana, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la Bwana. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu.

18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi.

19 “Mimi mwenyewe nilisema,

20 Lakini kama mwanamke asiye mwaminifu kwa mumewe,

21 Kilio kinasikika juu ya miinuko iliyo kame,

22 “Rudini, enyi watu msio waaminifu,

23 Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilima

24 Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala

25 Sisi na tulale chini katika aibu yetu,

Ler em outra tradução

Comparar lado a lado