1 Heri wale walio waadilifu katika njia zao,
2 Heri wale wanaozishika shuhuda zake,
3 Wasiofanya lolote lililo baya,
4 Umetoa maagizo yako
5 Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara
6 Hivyo mimi sitaaibishwa
7 Nitakusifu kwa moyo mnyofu
8 Nitayatii maagizo yako;
9 Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?
10 Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
11 Nimelificha neno lako moyoni mwangu
12 Sifa ni zako, Ee Bwana,
13 Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote
14 Ninafurahia kufuata sheria zako
15 Ninatafakari maagizo yako
16 Ninafurahia maagizo yako,
17 Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi;
18 Yafungue macho yangu nipate kuona
19 Mimi ni mgeni duniani,
20 Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa
21 Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa
22 Niondolee dharau na dhihaka,
23 Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia,
24 Sheria zako ni furaha yangu,
25 Nimelazwa chini mavumbini,
26 Nilikueleza njia zangu ukanijibu,
27 Nijulishe mafundisho ya mausia yako,
28 Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni,
29 Niepushe na njia za udanganyifu,
30 Nimechagua njia ya kweli,
31 Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana,
32 Nakimbilia katika njia ya maagizo yako,
33 Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako,
34 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako
35 Niongoze kwenye njia ya amri zako,
36 Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako,
37 Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa,
38 Mtimizie mtumishi wako ahadi yako,
39 Niondolee aibu ninayoiogopa,
40 Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako!
41 Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie,
42 ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki,
43 Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu,
44 Nitaitii amri yako daima,
45 Nitatembea nikiwa huru,
46 Nitasema sheria zako mbele za wafalme
47 kwa kuwa ninazifurahia amri zako
48 Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu,
49 Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako,
50 Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:
51 Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka,
52 Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani,
53 Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu,
54 Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu
55 Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako,
56 Hili limekuwa zoezi langu:
57 Ee Bwana, wewe ni fungu langu,
58 Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote,
59 Nimezifikiri njia zangu
60 Nitafanya haraka bila kuchelewa
61 Hata waovu wanifunge kwa kamba,
62 Usiku wa manane ninaamka kukushukuru
63 Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao,
64 Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako,
65 Mtendee wema mtumishi wako
66 Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri,
67 Kabla sijapata shida nilipotea njia,
68 Wewe ni mwema, unalotenda ni jema,
69 Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo,
70 Mioyo yao ni katili na migumu,
71 Ilikuwa vyema mimi kupata shida
72 Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu
73 Mikono yako ilinifanya na kuniumba,
74 Wakuchao wafurahie wanaponiona,
75 Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki,
76 Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu,
77 Huruma yako na inijie ili nipate kuishi,
78 Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu,
79 Wale wakuchao na wanigeukie mimi,
80 Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako,
81 Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako,
82 Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako;
83 Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi,
84 Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini?
85 Wenye majivuno wananichimbia mashimo,
86 Amri zako zote ni za kuaminika;
87 Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia,
88 Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako,
89 Ee Bwana, neno lako ni la milele,
90 Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote,
91 Sheria zako zinadumu hadi leo,
92 Kama nisingefurahia sheria yako,
93 Sitasahau mausia yako kamwe,
94 Uniokoe, kwa maana mimi ni wako,
95 Waovu wanangojea kuniangamiza,
96 Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo,
97 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.
98 Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,
99 Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,
100 Nina ufahamu zaidi kuliko wazee,
101 Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya,
102 Sijaziacha sheria zako,
103 Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu,
104 Ninapata ufahamu kutoka mausia yako,
105 Neno lako ni taa ya miguu yangu
106 Nimeapa na nimethibitisha,
107 Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana,
108 Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu,
109 Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote,
110 Waovu wamenitegea mtego,
111 Sheria zako ni urithi wangu milele,
112 Nimekusudia moyoni mwangu
113 Ninachukia watu wa nia mbili,
114 Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu,
115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya,
116 Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi;
117 Nitegemeze, nami nitaokolewa,
118 Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako,
119 Waovu wa nchi unawatupa kama takataka,
120 Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe,
121 Nimetenda yaliyo haki na sawa,
122 Mhakikishie mtumishi wako usalama,
123 Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako,
124 Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako
125 Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu
126 Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia,
127 Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu,
128 na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili,
129 Sheria zako ni za ajabu,
130 Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,
131 Nimefungua kinywa changu na kuhema,
132 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote
133 Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako,
134 Niokoe na uonevu wa wanadamu,
135 Mwangazie mtumishi wako uso wako
136 Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu,
137 Ee Bwana, wewe ni mwenye haki,
138 Sheria ulizoziweka ni za haki,
139 Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu
140 Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu,
141 Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa,
142 Haki yako ni ya milele,
143 Shida na dhiki zimenipata,
144 Sheria zako ni sahihi milele,
145 Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote,
146 Ninakuita; niokoe
147 Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada;
148 Sikufumba macho yangu usiku kucha,
149 Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako,
150 Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami,
151 Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu,
152 Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako
153 Yaangalie mateso yangu, uniokoe,
154 Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe,
155 Wokovu uko mbali na waovu,
156 Ee Bwana, huruma zako ni kuu,
157 Adui wanaonitesa ni wengi,
158 Ninawatazama wasioamini kwa chuki,
159 Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako;
160 Maneno yako yote ni kweli,
161 Watawala wamenitesa bila sababu,
162 Nafurahia ahadi zako
163 Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo,
164 Ninakusifu mara saba kwa siku,
165 Wanaopenda sheria yako wana amani tele,
166 Ee Bwana, ninangojea wokovu wako,
167 Ninazitii sheria zako,
168 Nimetii mausia yako na sheria zako,
169 Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako,
170 Maombi yangu na yafike mbele zako,
171 Midomo yangu na ibubujike sifa,
172 Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako,
173 Mkono wako uwe tayari kunisaidia,
174 Ee Bwana, ninatamani wokovu wako,
175 Nijalie kuishi ili nipate kukusifu,
176 Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea.