Jeremias 22

SWHONEN

1 Hili ndilo asemalo Bwana: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, utangaze ujumbe huu huko:

2 ‘Sikia neno la Bwana, ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi: wewe, maafisa wako na watu wako mnaopitia malango haya.

3 Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

4 Kwa kuwa ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi, huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao.

5 Lakini kama hutayatii maagizo haya, asema Bwana, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ”

6 Kwa kuwa hili ndilo Bwana asemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:

7 Nitawatuma waharabu dhidi yako,

8 “Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’

9 Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ”

10 Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;

11 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena.

12 Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.”

13 “Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,

14 Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,

15 “Je, inakufanya kuwa mfalme

16 Aliwatetea maskini na wahitaji,

17 “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu

18 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

19 Atazikwa maziko ya punda:

20 “Panda Lebanoni ukapige kelele,

21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,

22 Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,

23 Wewe uishiye Lebanoni,

24 “Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo.

25 Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo.

26 Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko.

27 Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”

28 Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa,

29 Ee nchi, nchi, nchi,

30 Hili ndilo Bwana asemalo:

Ler em outra tradução

Comparar lado a lado