Jeremias 17

SWHONEN

1 “Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma,

2 Hata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao

3 Mlima wangu katika nchi pamoja na utajiri

4 Kwa kosa lako mwenyewe utaupoteza

5 Hili ndilo asemalo Bwana:

6 Atakuwa kama kichaka cha jangwani;

7 “Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika Bwana,

8 Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji

9 Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote,

10 “Mimi Bwana huchunguza moyo

11 Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga,

12 Kiti cha enzi kilichotukuzwa, kilichoinuliwa tangu mwanzo,

13 Ee Bwana, uliye tumaini la Israeli,

14 Uniponye, Ee Bwana, nami nitaponyeka;

15 Wao huendelea kuniambia,

16 Sijakukimbia na kuacha kuwa mchungaji wako;

17 Usiwe kwangu kitu cha kunitia hofu kuu;

18 Watesi wangu na waaibishwe,

19 Hili ndilo Bwana aliloniambia: “Nenda ukasimame kwenye lango la watu, mahali ambako wafalme wa Yuda huingilia na kutokea, simama pia kwenye malango mengine yote ya Yerusalemu.

20 Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, nanyi watu wote wa Yuda, na kila mmoja aishiye Yerusalemu apitaye katika malango haya.

21 Hili ndilo asemalo Bwana: Jihadharini msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, wala kuingiza mzigo kupitia malango ya Yerusalemu.

22 Msitoe mizigo nje ya nyumba zenu wala kufanya kazi yoyote wakati wa Sabato, lakini itakaseni siku ya Sabato, kama nilivyowaamuru baba zenu.

23 Hata hivyo hawakusikiliza wala kujali, walishupaza shingo zao, na hawakutaka kusikia wala kukubali adhabu.

24 Lakini mkiwa waangalifu kunitii, asema Bwana, nanyi msipoleta mzigo wowote kupitia malango ya mji huu wakati wa Sabato, lakini mkaitakasa siku ya Sabato kwa kutofanya kazi siku hiyo,

25 ndipo wafalme wakaao juu ya kiti cha enzi cha Daudi wataingia kupitia malango ya mji huu, pamoja na maafisa wao. Wao na maafisa wao watakuja wakiwa wamepanda magari na farasi, wakiandamana na watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, nao mji huu utakaliwa na watu daima.

26 Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na chini ya vilima vya magharibi, kutoka nchi ya vilima na Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na dhabihu, sadaka za nafaka, uvumba na sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Bwana.

27 Lakini ikiwa hamtanitii mimi kwa kuitakasa Sabato na kwa kutochukua mzigo wowote mnapoingia katika malango ya Yerusalemu wakati wa Sabato, basi nitawasha moto usiozimika katika malango ya Yerusalemu utakaoteketeza ngome zake.’ ”

Ler em outra tradução

Comparar lado a lado