Isaías 38

SWHONEN

1 Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

2 Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana:

3 “Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.

4 Ndipo neno la Bwana likamjia Isaya, kusema:

5 “Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako. Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako.

6 Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

7 “ ‘Hii ndiyo ishara ya Bwana kwako ya kwamba Bwana atafanya kile alichoahidi:

8 Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.

9 Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona:

10 Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu,

11 Nilisema, “Sitamwona tena Bwana,

12 Kama hema la mchunga mifugo,

13 Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,

14 Nililia kama mbayuwayu au korongo,

15 Lakini niseme nini?

16 Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,

17 Hakika ilikuwa ya faida yangu

18 Kwa maana kaburi haliwezi kukusifu,

19 Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,

20 Bwana ataniokoa,

21 Isaya alikuwa amesema, “Tengenezeni dawa ya kubandika ya tini, mweke juu ya jipu, naye atapona.”

22 Hezekia alikuwa ameuliza, “Kutakuwa na ishara gani kwamba nitapanda kwenda Hekalu la Bwana?”

Ler em outra tradução

Comparar lado a lado