Esdras 2

SWHONEN

1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,

2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):

3 wazao wa Paroshi

4 wazao wa Shefatia

5 wazao wa Ara

6 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu)

7 wazao wa Elamu

8 wazao wa Zatu

9 wazao wa Zakai

10 wazao wa Bani

11 wazao wa Bebai

12 wazao wa Azgadi

13 wazao wa Adonikamu

14 wazao wa Bigwai

15 wazao wa Adini

16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia)

17 wazao wa Besai

18 wazao wa Yora

19 wazao wa Hashumu

20 wazao wa Gibari

21 watu wa Bethlehemu

22 watu wa Netofa

23 watu wa Anathothi

24 watu wa Azmawethi

25 wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi

26 wazao wa Rama na Geba

27 watu wa Mikmashi

28 watu wa Betheli na Ai

29 wazao wa Nebo

30 wazao wa Magbishi

31 wazao wa Elamu ile ingine

32 wazao wa Harimu

33 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono

34 wazao wa Yeriko

35 wazao wa Senaa

36 Makuhani:

37 wazao wa Imeri

38 wazao wa Pashuri

39 wazao wa Harimu

40 Walawi:

41 Waimbaji:

42 Mabawabu wa lango la Hekalu:

43 Watumishi wa Hekalu:

44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,

45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,

46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,

47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,

48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,

49 wazao wa Uza, Pasea, Besai,

50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,

51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

54 wazao wa Nesia na Hatifa.

55 Wazao wa watumishi wa Solomoni:

56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.

58 Watumishi wa Hekalu wote na // wazao wa watumishi // wa Solomoni

59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

60 wazao wa // Delaya, Tobia na Nekoda

61 Kutoka miongoni mwa makuhani:

62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.

63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.

64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;

65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.

66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,

67 ngamia 435 na punda 6,720.

68 Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.

69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.

70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

Ler em outra tradução

Comparar lado a lado